Taarifa kwa wanachama

Taarifa kwa wanachama

Ndugu Wanachama,

Katika kutimiza lengo la kupata wanachama 1milioni na baadae 3milioni ifikapo mwaka 2024, * Sisi ni taasisi ya Kitaifa na kutambua hilo Ofisi ya Rais wa TRCS imefanikiwa kupata udhamini wa nafasi 1,500 za vijana chini ya miaka 35 wa kuvoluntia kwenye chama chetu watakaolipwa 150,000/= nauli na posho kila mwezi na udhamini huu ni muhimu tukautumia vema kujipanga zaidi na kupata wanachama wapya*. Hii ina maana kwamba kwa wastani kila Wilaya nchi nzima ni zaidi ya Vijana 10.  Na ikumbukwe TRCS haitohusika na kuwalipa vijana hao malipo hayo kila Mwezi.

Majukumu yao makuu yatakuwa ni pamoja na;-

1) Kutafuta na kuwasajili kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa husika wanachama na voluntia wengi zaidi wa TRCS.

2) Kutoa hamasa ya watanzania wengi zaidi kutambua majukumu ya msingi ya TRCS.

3) Kuongeza mahusiano ya kiutendaji kati ya TRCS na Viongozi wa serikali hususani vijiji, Kata na Wilaya

4) Kukusanya takwimu zingine muhimu za TRCS watakazo elekekwa na viongozi wa Mkoa na Kitaifa.

5) Kutoa elimu ya huduma ya kwanza na elimu ya kujikinga na majanga mbali mbali.

NB:- Vijana hawa wanapaswa kuwa wanatokea ktk maeneo hayo wanayofanyia kazi ili iwe rahisi kutimiza malengo ya kila voluntia kupata wanachama angalau 10 kwa siku.

WITO:

Viongozi wa Mikoa mnatakiwa kuwatafuta vijana hao na watapewa maelekezo zaidi. Jukumu letu viongozi ni kuhakikisha tunawapata hao vijana kabla ya tarehe 30.10.2019 ili waanze majukumu yao tarehe 01.11.2019.

SIFA ZA VIJANA HAO:

  1. Elimu ngazi ya Degree yeyote kutoka chuo kinachotambulika na serikali.
  2. Elimu ngazi ya Diploma ni LAZIMA iwe Diploma ya Ualimu kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
  3. Awe ni mkazi wa eneo husika kwa zaidi ya miaka mitatu hadi sasa-uthibitisho utolewe na uongozi wa serikali ya mtaa/kata wa eneo husika.

SAMAHANI MAOMBI YAMEFUNGWA KWA SASA

MAWASILIANO:

Focal person wa jambo hili ni hivyo ukiwa na swali zaidi tafadhali muulize au uliza kwa Katibu Mkuu au Mhe. Rais wa TRCS moja kwa moja.

Iwapo ataulizwa au kuomba hela ada yoyote, Unaombwa atoe taarifa kwa Tanzania Red Cross – kupitia kwa Ndugu Reginald Mhango-0754 800 003 au barua pepe Rasmi ya shirika: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. Pia Tanzania Red Cross Haipokei maombi kwa mfumo wa Gmail bali kwa Kiungo(Link) iliyokuja na ujumbe huu.

Tanzania Red Cross Society (TRCS) HAIDAI MALIPO YOYOTE katika hatua yoyote ya mchakato wa kuajiri. Maombi yote ni ya bure kwa wagombea wote na hakuna mtu anayepaswa kulipa malipo au fidia wakati wa mchakato wa kuajiri.

Asanteni sana.