Waziri Afananisha TRCS na Usalama wa Taifa

Waziri Afananisha TRCS na Usalama wa Taifa

Waziri wa Katibana Sheria, Balozi Augustine Mahiga, alifungua Mkutano  Mkuu wa Uchaguzi wa Tanzania Red Cross Society kikiwa na ajenda kuu ya uchaguzi wa viongozi watakaokiongoza kwa miaka mitano ijayo.

Amefananisha majukumu ya Tanzania Red Cross   Society na yale ya Idara ya Usalama wa Taifa;

na ili kiendelee kudumisha hadhi yake na awamu hii amewataka kuchagua vijana. “Niliwahi kuwa mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa, enzi za Mwalimu (Hayati baba waTaifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere) akawa anasema kazi ya idara hiyo siyo tu kunusanusa kuchongea chongea,” amesema na kuendelea,                 

“Kazi yake ni kusaidia serikali iwe serikali bora, kwa kutoa taarifa na ushauri ambao utawezesha viongozi kutoa maamuzi sahihi, ambayo yatanufaisha wananchi.”

Alisema chama hicho kinaposaidia serikali ikatoa huduma bora hususan kwenye eneo la huduma za afya, kinakuwa kimeiwezesha kuwa serikali bora, inayokubalika kwa watu kwani ubora wa serikali hupimwa kwa ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Alisema anakifahamu vizuri chama kwakuwa amewahi kukitumikia kwa miaka 11 na amekielezea  kuwa ni kikongwe,  chenye mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

Aliwahimiza Wajumbe wa Mkutano huo, kuendelea kuchagua viongozi waliopikwa na kuwiva katika misingi ya chama hicho

“Hiki ni chama chenye misingi, taratibu, heshima,  malengo, miiko na  sura ya kimataifa hivyo lazima mchaguane mkilenga kudumisha na kuimarisha mambo hayo ndani ya Taifa letu,” amesema Balozi Mahiga.

Naye Mwenyekiti wa Tanzania Red cross Tanzania, Mwadini Jecha, ameshukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali kwa kuwezesha uwepo wa sheria ambayo inakipa nguvu zaidi  chama hicho katika kutimiza majukumu yake ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, alisema dunia ina watu wengi sana lakini binadamu ni wachache na kwamba uhalisia wakauli hiyo unabainika unaporejea idadi ya wanachama wa Tanzania Red Cross nchini ambao hufanya kazi zao wakiongozwa na nguvu ya ubinadamu.

                                                                

“Shughuli za chama hiki zinajikita katika misingi ya ubinadamu, watu wanajitolea kuhudumia wengine bila kutarajia faida na ndiyo maana idadi ya wanachama wa Chama hiki nchini hawafikii hata Mil. 1 wakati jumla ya watanzania ni zaidi ya Milioni 40,” alisema DC Katambi.

                    

Siku ya pili ya Mkutano huo ilifunguliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson

Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambapo alishauri TRCS kufungua matawi mengi zaidi na imara yenye wanachama wakutosha ili huduma wanazozitoa ziwafikie watu wengi zaidi.

Naibu Spika Dkt Tulia alisema matawi hayo yatasaidia kutoa elimu kuhusiana na Shirika hilo kwa wananchi wengi zaidi ili waweze kujua majukumu ya Shirika na vilevile kuwajengea uzalendo na jinsi ya kufanya shughuli za kujitolea.

“Niwapongeze pia kwa kuanzisha Baraza la Vijana , niwatie moyo wa kuendelea na mkakakati wenu wa kuwashawishi vijana wengi zaidi wajiunge na taasisi yenu kupitia klabu za vijana mashuleni, vijana ndiyo nguvu kazi ambayo ikitumiwa vizuri basi mtachangia kujenga jamii bora yenye kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii,” alisema.

Aidha, alilitakaTanzania Red Cross kuzingatiaKanunisabazakibinadamu, uadilifu, kutopendelea, uhuru, kujitolea, umojanaushirikiano.

“Kwa kufanya hivyo mtakuwa mnajenga Taasisi imara ambayo inaaminiwa na kuheshimika mbele ya Serikali, wadau mbalimbali najamii kwa ujumla,” alisema

Alisema Bunge limeifanyia marekebisho mara kwa mara sheria iliyoanzisha Shirika hilo ili kuipa nguvu na kuliwezesha kutimiza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kwamba Bunge lipo tayari kuendelea kushirikiana na Shirika hilo.

Katika Mkutano huo Naibu Spika alikubali ombi la kuwa Balozi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania na kuahidi kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu na unyenyekevu mkubwa.

Rais wa Awali Shirika hilo, Ndugu David Kihevile alimshukuru Naibu Spika kwa kukubali kuwafungulia Mkutano wao .

                       

Alieleza majukumu ya chama kwamba ni kutoa huduma mbalimbali za kibinadamu na kwamba Shirika hilo lingetamani kila Mtanzania awe na moyo wa ubinadamu wakusaidia jamii ya watu wanyonge.

Katika Mkutano huo Naibu Spika alitunikiwa uanachama wamaisha na kuwa balozi wa Tanzania Red Cross society.

Tanzania Red Cross Society yapata viongozi wapya.             

Viongozi waliochaguliwa wanaunda Halmashauri Kuu ya TRCS Taifa ambayo inahusika na majukumu ya usimamizi wa jumla wa shughuli za Tanzania Red Cross Society. Viongozi waliochaguliwa ni:

Jina

Nafasi

David Mwakiposa Kihenzile

Rais

Lucia Pande

MakamuwaRais

Japhet Shirima

MwekaHazina

Herman Kashililika

MshauriwaMipango

Felician Mhongerwa

MshauriwamasualayaMaafa

Dr. Florence Ndaturu Siyame

MshauriwaAfyanaMafunzo

Nuru Ali  Liyau

MshauriwaJinsia

Robert J. Kayoka

Muwakilishiwa Kanda yaZiwa

Shaban S. Mloti

Muwakilishiwa Kanda yaMagharibi

Ester E. Maleko

Muwakilishiwa Kanda ya Kanda yaKaskazini

Bryton Mkwambe

Muwakilishiwa Kanda yaNyandazaJuuKusini

Dollar  Kussenge

Muwakilishiwa Kanda yaMashariki

Tryphone Mkolokoti

Muwakilishiwa Kanda ya Kati

Zuberi  Khamis

Muwakilishiwa Kanda ya Zanzibar

Rahim  Khamis  Kalyango

MwenyekitiwawaBaraza la VijanaTaifa (Mjumbekwanafasiyake)

Wajumbe wawili wa kuteuliwa ni Ndg. Christopher Nzella na Ndg. Jamal Kassim Ali.

Rais Mwakiposa aelezea vipaumbele

Vipaumbele vya Rais Mpya wa Tanzania Red Cross Society vimejikita katika makundi matatu ya Uanachama, miradi na nidhamu.

                                           

Akizungumza na wajumbe alisema ‘’Sote tunaamini katika maono, mikakati na matokeo, kujenga taasisi inayowajibika na kuheshimika na wadau wote katika jamii kama kisaidizi cha serikali.

“Tunataka kujenga taasisi ambayo inamikakati inayotekelezeka na kuwa chama kinachojitegemea na kupunguza utegemezi, ili kumuenzi mlezi wa chama kwa vitendo ambaye aliamini  katika kujitegemea.” Alisema Rais Mwakiposa

Pia alisema vipaumbele vingine ni kuunda kamati ndogo itakayoenda kufuatilia mali zote za chama popote zilipo ili kujua tunamiliki nini, Kujenga chama ambapo chama kitataka kujua  kuna mikataba mingapi na inahusu nini na je makubalino hayo yana faida gani kwa Tanzania red Cross hata inayohusu watumishi.

Aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni Kujenga chama kinachotekeleza maazimio yanayotolewa na vikao vyote na kupata taarifa ya utekelezaji, Kujenga taasisi yenye nidhamu na viongozi wake wanajiheshimu na watekeleze majukumu yao kwa taratibu zilizopo watu wajipime sehemu walipo na majukumu yao, watu wafanye kazi kwa matokeo. Kuanzia viongozi wa juu, watendaji na Taifa

‘’Tunataka kufanya uchambuzi wa wafadhili na wadau ili kujua wadau na washirika wa maendeleo ni wepi na wawepo kwenye kanzi data kuanzia ngazi ya tawi, Mkoa naTaifa. Alieleza.

                      

‘’Vile vile tunatamani kujenga chama kinachoheshimu watangulizi wa Red Cross, Kujenga chama chenye wanachama wengi na ambao wanafanya kazi zinazowatangaza wenyewe, mfano inapotokea maafa watu wajue red cross ipo.’’ Aliendelea kusema.

Rais Mwakiposa hakusita kueleza changamoto ndani ya chama katika upande wa teknolojia ya habari na mawasiliano na kuahidi kwamba lazima kuwe na mfumo wa uhakika na  taasisi kujitangaza ili kuvutia watu zaidi. Kwakua  Tanzania Red Cross  imepata balozi mpya, imemuagiza pongezi  kwa kusaini sheria mpya, pia kumweleza kuwa Tanzania Red Cross imezaliwa upya.