Kigoma - TRCS: Katibu Mkuu Tanzania Red Cross Society akabidhi jengo la Damu Salama kwa Serikali wilayani Kasulu

Katibu Mkuu Tanzania Red Cross Society *Ndg.Felician Mtahengerwa*  akabidhi jengo la Damu Salama kwa Serikali lililojengwa kwa mradi wa Blood Safe Project, mradi unaosimamiwa na *Tanzania Red Cross Society* wilayani Kasulu mkoani Kigoma chini ya udhamini wa *Spanish Red Cross*.

Akabidhiwa jengo hilo Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Mhe.Rashid Mchatta ambaye ameishukuru sana TRCS kwa msaada huu na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanazofanya hasa wanapoiangalia Kigoma kwa ukaribu mkubwa kwani Kigoma imekua ndio mnufaika wa Tanzania Red Cross Society wakati wote.